|
KIITIKIO
Niamini -
sema
Nataka uwe na mimi - mama
Watu wenye fitina wanaleta majungu tuachane na mimi - yeyeyeeeee
Hivi kwanini - semaa
Hutaki kuniamini - mamaa
Nyoyo zipo pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi - yeyeyee
x 2
(verse 1)
Prof. J:
Nakupenda
sana ingawa wanakuita demu wa uswazini.
Penzi letu la kweli ndio kitu nachothamini.
Kipepeo cha moyo we sema unachotaka.
Jinsi unavyoenzi kipenzi sina mashaka.
Tulipanda milima tukaja kwenye mabonde.
Sasa ni tambarare tufanye wanga wakome
Kote tunakopita wamemwaga mbigili.
Njoo nikumbatie tufe tukiwa wawili.
Hushangai tukigombana tu wanafurahi.
Na tukiwa pamoja wanashindwa kutusabahi.
Walishakuja kwangu kunipa habari zako.
Nikawatowa mbio kulinda heshima yako.
Kwangu wamenishindwa wamegeuza kibao.
Changanua mapema upime akili zao.
Ni maisha yo Liz twende tujikongoje.
Maisha safari ndefu sijui mbele kukoje.
Wanasema mi nakunywa weee nalala kwenye Bar.
Wanaema mi ni bingwa la ngono kwenye mitaa
Wanasema mi nimeshawataka wamekataa
Kwako napiga goti yo twende kisuperstar
KIITIKIO
(verse
2)
BIG WILLY:
Yoo
ni kwamba mi nashukuru sana, umenimini kwa sana
Hukufuata maneno ya wanga waliochanganya kwa sana.
Miss Mangana babu kubwa hiyo ni dhana.
Wala hukunikana aksante sana mi sitokukana Hatukufarakana tulikaa chini
tukapatana bila kugombana
Na ndio maana hatujatengana tukasameheana bila Kutosana endelea kukazana
vizabizabina maji ya shingo sasa chupi zinawabana vichwa vinagongana hatujaachana
Wanapigwa na bumbuwazi wanapoona bado tunakumbatiana
Tunashirikiana na tunafanya vitu vya maana, na haki ya Mungu nakuahidi
mi ndoa dhamana nakata mzizi wa fitina
Wewe ni wangu wa kuzikana, wengine hakuna vitonge Manyoya, sasa hapana
kwani maneno yalizidi kutoka kwa Wanga na mahasidi na wengine waliahidi
lazima Tummwagie asidi, eti wa mkono wakutupwa na ninapiga Sana mchupa,
hautachukua raundi kwangu mimi nitakutupa
Haukufanya pupa haukuogopa ukajitosa,
Ya mungu mengi leo hii kwetu mambo ni supa
Na yote ndio niliyoahidi kwako lazima mi nitakupa
Usiwe na pupa tulia mi ndio simba unanipa hamu na hilo
Napenda ufahamu, na ninakumbuka maneno yako matamu
"Mi nakupenda wewee" unanipa kiwewe
Ubavu wangu wa pili ni wewe,
Napenda uelewe ni mimi na wewe tu.
KIITIKIO
(verse
3)
Fanani Terry:
Amini
amini tupo safarini, wala sigeuki nipo makini
Na wenye chuki hivi hujabaini, wanakudanganya
Maneno lukuki eti napenda chini, eti nakuasi na
Hugutuki hivi inaingia akilini, ni muda gani na nilini Sinyo Hatukuwa
pamoja kama si uzushi ni nini wanga Wanajikongoja, ninavyokupenda kwa
ukaraha ndio maana Wametunga hoja tutengane iwe furaha ili watuzushie
vioja Usiwaamini mara moja wengi ni vizabizabiana
Wapiga majungu na fitina magwiji washirikina
Pima vyema tena kwa kina, tusije tukaachana
Tutawapa msemo wakenue meno, itakuwa haina
Maana mara tu tumefarakana bibie itakuwa aibu
Tujaribu kuvumilia penzi ni taratibu
Mambo ya jana sio ya leo tusije tukaaribu
Hebu sikia sogea karibu nani wakunighiribu
Kwako sioni sisikii ukiacha utaniadhibu
Wewe nipo, raha nipe zabibu mpaka nitakapokufa
Tushirikiane kuziba ufa wanga wasitufuate
Nafurahi unavyonipenda Sinyo nasema aksante
We nipe denda nipe mate mama subiri fungate
Mzizi wa fitina mpaka tuukate
Wewe na mimi nipo radhi kula yamini
Wewe na mimi mama Ray niamini
KIITIKIO
|
|