Mwanafalsafa - Ingekuwa vipi ?  
     
 

(verse 1)
Mwanafalsafa:
Ingekuwa vipi angekuwa hai D-Rob?
Na Chief Ramso angekuwa Bongo?
Wahisani bila kidato?
Na umrudishe K-Single?

(verse 2)
Kwanza ingekuwa mfano?
Au tayari ingekuwa chongo?
Kati ya nani angekuwa uigo?
Na nani angebaki mzigo?

(verse 3)
Mr II
:Ingekuwa vipi balozi na Mr.II?
Mwanafalsafa: Mr. II!
Mr II: Wafanye vita ulingoni siseme su?
Mwanafalsafa: seme su!
Mr II: Unajua nani kati yao angeibuka mikono juu?
Sema nani kati yao angeibuka mikono juu!

(verse 4)
Mwanafalsafa: Ingekuwa vipi Dully Sykes angeimba Hardcore?
Mashairi kama Jay Mo?
Neno wanasesere n'na imani lisingekuwepo.
Mauzo ya Rap ya bongo yangefika Platinum tano;
Mr II: Mauzo ya rap ya bongo yangefika Platinum tano!

(verse 5)
Mwanafalsafa:Ingekuwa vipi HBC bila Jay?
Mr II: Bila Jay!
Ingekuwa sawa na The Wailers bila Marley.
Mwanafalsafa: Bila Marley!
Mr II: Hiyo ni sawa kuwepo Snoop bila Dre.
Mwanafalsafa: Bila Dre!
Mr II: Makumbusho bila kijiji au Bongo bila Nyerere.

(verse 6)
Mwanafalsafa: Ingekuwa vipi, maisha ya Temeke yangekuwa juu kidogo?
Unadhani wasanii wangejiita walume ndago?
Mr II: Ingekuwa vipi Bongo Records isingekuwa ya Halfani?
Watu kama flani-flani tusingewasikia hewani!

(verse 7)
Mwanafalsafa: Angeimba nini Sister P, asingekuwepo Zay B?
Mr II: Na ingekuwa wapi R&B asingekuwepo Jay D ?
x2


KIITIKIO

Mwanafalsafa: Nawaza mambo kwa kina
Na bado majibu sina
Uwezo wa Mungu unaonekana
Angeamua ingewezekana

Mr II: Nawaza mambo kwa kina
Na bado majibu sina
Uwezo wa Mungu unaonekana
Angeamua ingewezekana!

Mwanafalsafa: Ingekuwa vipi?
Mr II: Ingekuwa vipi?
x8


(verse 8)
Mwanafalsafa
: Ingekuwa vipi Bongo mitumba isingehalalishwa?
Masista Du pedal-pusher vipi wangeshonesha?
Mr II: Vitovu wangetuonyesha?
Je mapozi yangekwisha?
Au pigo gani brother-man leo zingemdatisha?

(verse 9)
Mwanafalsafa: lngekuwa vipi bongo wasingekuwepo changudoa?
Wateja wao, je wangewaopoa makaka poa?
Mr II: Au pengine matendo ya ubakaji yangewaingia?
Au labda ni masterbeshen ndizo zingewaokoa?

(verse 10)
Mwanafalsafa: Ingekuwa vipi kasi ya Ukimwi kusingekuwa Condoms?
Yani ingekuwaje bila Ukimwi tungetinga Condoms?
Au Ukimwi ungekuwepo halafu hakuna Condoms
Unadhani mi ningesema mimi na mabinti ni dam-dam?

(verse 11)
Mr II: lngekuwa vipi ulipe buku tu kwa kila pumzi?
Kiumbe gani angediriki leo kupiga mluzi?
Unadhani ni watu wangapi wangekuwa wazima?
Labda tajiri, mafukara si tusingepona!

(verse 12)
Mwanafalsafa: Ingekuwa vipi kama Bongo ingekuwa kama New York?
Washikaji wangejazana ubalozini kuomba viza?
Au viza tungezipata bila ya kuongea Kiingereza?
Kama sio chizi utawaza, maswali mi najiuliza.
Ingekuwa vipi?

KIITIKIO

(verse 13)
Mwanafalsafa
: Ingekuwa vipi Yesu angerudi?
Angemaliza vita ya Wapalestina na Wayahudi?
Fikiri ungeisha vipi mgogoro wa nchi ya ahadi?
Na fikiri uwepo wake ungeokoa maisha ya wangapi?

(verse 14)
Mr II
: lngekuwa vipi kama Osama angeutawala Ulimwengu?
Wamarekani Uarabuni wangekuwa Sungusungu?
Je magaidi wangekuwa nani, ma-black au Wazungu?
Waarabu wangeelimika, wangetoka kwenye ukungu?

(verse 15)
Mwanafalsafa
: Ungekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini?
Dunia bila dhambi,Kipimo cha uovu nini?
Polisi, mahakama na gerezani angeenda nani?
Huitaji dini tathmini ingekuwa vipi hali ya amani?

(verse 16)
Mr II
: Vipi kama duniani wangekuwa ni mabinti peke yao?
Je wangetembea uchi kwa sababu hakuna wenzao?
Au wangejisitiri! Mitindo ingekuwa ya nini?
Ya kazi gani kama hakuna wanaume duniani?

(verse 17)
Mwanafalsafa
: Vipi kama Wazungu wasingeingia Afrika?
Nadhani maendeleo kwetu yangechelewa kufika.
Magari, ndege, Reli na nguo, nani angeleta?
Na bila biashara ya utumwa wangekuwepo black Amerika?
ah ha?

KIITIKIO x 2

 
     
  Lyrics by Liyoya Group  
     
  © mzibo.net